JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MKATABA WA KUKODISHA VIFAA / MITAMBO
Mkataba huu umefanywa leo tarehe [ ] mwezi wa [ ], [MWAKA] kati ya:
[JINA LA MMILIKI], NIDA / TIN Na. [ ], wa [ANWANI] (“Mkodishaji”); NA
[JINA LA MKODISHWA], NIDA / TIN Na. [ ], wa [ANWANI] (“Mkodishwa”).
Vifaa
| Aina ya kifaa | [mf. jenereta, mchanganyiko wa zege, kiunzi (scaffolding), trekta, vifaa vya sherehe] |
| Chapa / modeli / namba ya utambulisho | [ ] |
| Idadi | [ ] |
| Hali wakati wa kukabidhi | [ ] |
| Thamani ya kubadilisha (replacement value) | TSh [ ] |
Masharti
1. Muda: Kuanzia [tarehe na saa] hadi [tarehe na saa]. Kuchelewa kurudisha kutatozwa kodi ya ziada ya TSh [ ] kwa siku.
2. Kodi: TSh [ ] kwa [saa / siku / wiki / mwezi], inayolipwa [mapema / kila wiki]. [Mafuta na vilainishi ni juu ya Mkodishwa.]
3. Amana: Mkodishwa analipa amana ya TSh [ ], itakayorudishwa ndani ya siku [3] baada ya kurudisha vifaa vikiwa salama, baada ya kutoa gharama za uharibifu au kodi inayodaiwa.
4. Matumizi: Vifaa vitatumika tu katika [MAHALI] kwa kazi ya [ ], na mtu mwenye ujuzi. Mkodishwa hatavikodisha kwa mtu mwingine wala kuvihamisha bila idhini ya maandishi.
5. Mwendeshaji: [Mkodishaji atatoa mwendeshaji kwa malipo ya TSh [ ] kwa siku, ambaye atabaki chini ya maelekezo ya Mkodishwa kazini / Mkodishwa atatumia mwendeshaji wake mwenye ujuzi].
6. Matunzo: Mkodishwa atafanya ukaguzi wa kila siku (mafuta, maji, upepo) na kumjulisha Mkodishaji mara moja kifaa kikiharibika. Matengenezo makubwa yatafanywa na Mkodishaji, isipokuwa uharibifu umesababishwa na matumizi mabaya ya Mkodishwa.
Sehemu iliyobaki ya hati imefungwa
Lipa mara moja kwa simu na upakue hati kamili papo hapo.
Fungua kuanzia TSh 1,500