JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MKATABA WA WAKALA WA MAUZO
Mkataba huu umefanywa leo tarehe [ ] mwezi wa [ ], [MWAKA] kati ya:
[JINA LA KAMPUNI / MWENYE BIDHAA AU HUDUMA], TIN Na. [ ], wa [ANWANI] (“Mkuu”); NA
[JINA LA WAKALA], NIDA / TIN Na. [ ], wa [ANWANI] (“Wakala”).
Masharti
1. Uteuzi: Mkuu anamteua Wakala kutafuta wateja na kupokea maagizo ya [bidhaa / huduma] zilizoorodheshwa katika Jedwali, katika [ENEO / kundi la wateja].
2. Mamlaka: Wakala atatafuta na kuwasilisha maagizo kwa Mkuu, ambaye ana uhuru wa kuyakubali au kuyakataa. Wakala hana mamlaka ya kusaini mikataba, kubadilisha bei, kutoa punguzo au ahadi kwa niaba ya Mkuu bila idhini ya maandishi.
3. Muda: Kuanzia [ ] kwa miezi [ ], unaoweza kuongezwa.
4. Kamisheni: Wakala atalipwa kamisheni ya [ ]% ya thamani ya mauzo [bila VAT] ya kila agizo alilolileta na kukubaliwa, inayolipwa ndani ya siku [14] baada ya Mkuu kupokea malipo kutoka kwa mteja. Hakuna kamisheni kwa mauzo yasiyolipwa.
5. Fedha za wateja: Wakala hatapokea fedha za wateja isipokuwa ameidhinishwa kwa maandishi; malipo yote yatafanywa moja kwa moja kwenye akaunti ya Mkuu: [ ]. Fedha yoyote itakayopokelewa itawasilishwa ndani ya saa [24] na stakabadhi kutolewa.
Sehemu iliyobaki ya hati imefungwa
Lipa mara moja kwa simu na upakue hati kamili papo hapo.
Fungua kuanzia TSh 2,000